Kuwaomba uokozi maiti ni shirki kubwa

Swali: Je, inajuzu kuomba uokozi kutoka kwa Mitume, mawalii na watu wema katika uhai wao na baada ya kufa kwao ili wazuie dhara na walete jambo la kheri na kutawassul vilevile katika hali hizo mbili [katika uhai wao na baada ya kufa kwao] ili watatue haja?

Jibu: Kuwaomba uokozi maiti miongoni mwa Mitume na wengineo haijuzu bali ni katika shirki kubwa.

Kuhusiana na kuomba uokozi kutoka kwa mtu aliye hai na aliye mbele yako ni sawa. Allaah (Subhaanah) amesema katika kisa cha Muusa:

فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

“Akamsaidia yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake.” (28:15)

Ama kuhusu kutawassul kwa walio hai au maiti miongoni mwa Mitume au wengine kwa dhati zao, haja zao au haki zao haijuzu. Bali ni katika Bid´ah na njia zinazopelekea katika shirki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/55)
  • Imechapishwa: 06/10/2020