Kuwaomba uokozi maiti na wasioonekana

Swali: Je, kuwaomba uokozi maiti na watu wasioonekana ni kufuru kubwa?

Jibu: Ndio, kuwaomba uokozi maiti au watu wasioonekana ni shirki kubwa inayomtoa mwenye kufanya hivo katika Uislamu. Amesema (Subhaanah):

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.” (23:117)

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

“Huyo basi ndiye Allaah Mola wenu, ufalme ni Wake pekee. Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, basi [wasingeliweza] kukujibuni na siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna atakayekujulisha kama Mwenye khabari zote.” (35:13-14)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/57)
  • Imechapishwa: 06/10/2020