Swali: Mwenye kufa na yuko na wake watano au zaidi ni muislmu ambaye tuna haki ya kumswalia baada ya kufa kwake ilihali tunajua maneno ya Allaah (Jalla Sha´nuh):

أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا

“Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia.” (02:85)

Jibu: Imani haithibiti mwa mwenye kutamka “Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” isipokuwa ikiwa kama ataitamka kwa Ikhlaasw kutoka kwenye moyo wake. Haizingatiwi mbele ya Allaah mpaka iwe hivyo. Kuhusiana na yule mwenye kuitamka duniani anataamiliwa matangamano ya muislamu hata kama atakuwa hakuitamka kwa Ikhlaasw. Sisi tunaangalia udhahiri na yaliyojificha tunamwaachia Allaah.

Ambaye anaitamka na akafanya mambo yenye kuitengua anakufuru. Kwa mfano mwenye kuhalalisha mambo yenye kujulikana fika [uharamu wake] katika Uislamu kama kuhalalisha uzinzi na kuwaoa Mahaarim. Miongoni mwa mambo yenye kuitengua ni kuacha swalah kwa kukusudia baada ya kufikishiwa maamrisho yake na kunasihiwa kwayo. Hii ndio kauli sahihi katika kauli za wanachuoni. Vilevile miongoni mwa mambo yenye kuivunja ni kuvaa hirizi isiyokuwa ya Qur-aan pamoja na kuamini kuwa inaathiri. Ama akiamini kuwa hirizi ni sababu tu ya kupona au inamlinda na jini na kijicho ni haramu na wala haitengui Uislamu. Lakini hata hivyo katika hali hiyo itakuwa inaingia katika shirki ndogo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwenye kutundika hirizi basi hatapata kuona haja yake kutimizwa na Allaah. Na mwenye kutundika kombe la pwani hatapata amani na utulivu kutoka kwa Allaah.”

Kuhusiana na kuvaa hirizi ya Qur-aan wanachuoni wametofautiana. Hata hivyo maoni yenye nguvu ni kwamba ni haramu kutokana na ujumla wa dalili na kwa ajili ya kufunga njia inayopelekea katika kuvaa hirizi nyenginezo. Miongoni mwa mambo vilevile yanayotengua Uislamu ni kuwaomba uokozi maiti, masanamu na vitu visivyokuwa na uhai wa dhahiri miongoni mwa majina na watu au viumbe vilivyo hai na visivyokuwa mbele yako kwa mambo yasiyowezwa na yeyote isipokuwa Allaah pekee.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/50)
  • Imechapishwa: 06/10/2020