Kuwaletea watoto vipumbazo nyumbani ili wasiende nje

Swali: Leo njia za michezo zimekuwa nyingi ikiwa ni pamoja na TV, kompyuta, play station na vinginevyo. Ndani ya vitu hivi kuna mambo yenye kukatazwa na ya haramu. Je, niwakataze wanangu kuchezea vitu kama hivi na kutokana na madhara yanayopatikana ndani yake? Lakini wakati huo huo naogopa hilo lisisababishe madhara makubwa zaidi wanangu wakaenda kucheza kwenye mabarabara na wakasuhubiana na watu wabaya nisiyowajua na hiyo ikawa ni sababu ya kuwakimbiza wanangu na Dini na kusema kuwa sisi tunawakataza kila kitu.

Jibu: Ndio, inatakiwa kuwakataza watoto na mambo haya. Hili ni jukumu la baba kwanza kisha ndio anafuatia mama. Wanatakiwa kushirikiana kwa kuwalea watoto. Wawakataze na njia za shari na wasiziingize kwenye nyumba yao. Wawe na subira juu ya hilo. Wawe na subira juu ya lawama za watoto na maudhui yao. Wasiwatii kwa madai yao ya kwamba wanawakataza kufanya hayo nyumbani na hilo likawapelekea wao kuingiza mambo haya nyumbani kwa hoja wasiende kwenye mabarabara. Ina maana mnataka kuwaharibu wakiwa nyumbani ili wasiharibike kwenye mabarabara? Faida itakuwa sasa iko wapi? Mnataka kuwaharibu wakiwa nyumbani ili wasiharibike kwenye mabarabara. Hapana, ee ndugu! Jenga nia na makusudio mazuri na Allaah (´Azza wa Jall) Atakusaidia. Kuwa ni mwenye subira juu ya hilo. Watishie [hayo] wanao na uwalee juu ya hilo. Waambie mambo haya wanangu si ya sawa na ni yenye kuchukiza. Wabainishie madhara yake. Hayo yatawafanya wao kuachana nayo. Ukiwalea juu ya hili na ukawakinaisha watayaacha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%202-%2011-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2015