Swali: Ambaye anamkonyeza mtu kwa njia ya kwamba mtu anaelewa…

Jibu: Haijalishi kitu hukumu ni moja. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ

”Maangamivu kwa kila mwenye kukebehi na kukejeli watu kwa ishara na vitendo, na kwa kila mwenye kufedhehesha kwa ulimi.”[1]

Ni yule ambaye anawatia watu mapungufu kwa kuwakashifu na kuwakejeli kwa ishara. Mara inakuwa kwa kunong´ona, mara nyingine inakuwa kwa kidole chake, macho yake, kichwa chake au kwa njia nyingine inayofahamika:

وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ

“Na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, wa kutwezwa. Mwingi wa kukashifu, mwenye kueneza umbea.”[2]

[1] 104:01

[2] 68:10-11

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23194/حكم-من-يعيب-الناس-بالهمز-واللمز-بالاشارة
  • Imechapishwa: 24/11/2023