Kuwa na shangazi ambaye ni mchawi

Swali: Mimi nina shangazi ambaye sina mawasiliano naye kwa kuwa ninakhofia asinifanyie uchawi au kunifanya nikatumia madawa ya kulevya na mvinyo. Je, nina dhambi kwa kutokuwa na mawasiliano na yeye?

Jibu: Ikiwa ni kweli na yuko kama jinsi ulivosema, wewe ni mwenye kupewa udhuru kutokuwa na mawasiliano naye kwa kuhifadhi dini yako. Ama ikiwa una shaka tu na huna uhakika, kuwa na mawasiliano naye. Haki yake ya udugu haianguki midhali hujui kuwa yuko katika sifa inayomtoa katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-5-11-1435.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015