Kuwa na furaha kwa matendo mema anayofanya mtu

Swali: Hupatwa na furaha kubwa baada ya kufanya matendo mema kama swalah na kusoma Qur-aan. Je, hili linajuzu? Ninakhofia kujiona kwa matendo yangu?

Jibu: Furaha sio kitu kinachotokamana na wewe. Ni kitu kinachotoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ni dalili ya kheri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ

“Sema: “Kwa fadhilah za Allaah na kwa rehema Yake basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.” (10:58)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015