Kuvunja msikiti na kuhamisha maeneo mengine

Swali: Kuna mtu amejenga msikiti mdogo kwenye ardhi yake. Baada ya muda fulani akataka kujenga majengo katika ardhi hiyohiyo alipojenga msikiti kwa njia ya kwamba atavunja msikiti na ajenge msikiti mwingine maeneo mengine. Ni ipi hukumu ya kubomoa kwake msikiti huo?

Jibu: Haja ikipelekea kuuhamisha, kwa mfano lengo la kupanua, basi hapana neno kufanya hivo baada ya kurudi serikalini juu ya jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 22/08/2021