Kunyanyua kichwa wakati wa adhaana

Swali: Mtunzi wa “az-Zaad” amesema:

“Imesuniwa akanyanyua kichwa chake wakati wa adhaana.”

Je, ipo dalili au Athar juu ya jambo hilo?

Jibu: Imepokelewa katika baadhi ya mapokezi kwamba afanye hivo baada ya kutawadha kisha aombe du´aa. Kuhusu kunyanyua kichwa wakati wa adhaana sijui msingi wa hilo. Anachotakiwa ni kuelekea Qiblah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 22/08/2021