Kuvaa pete ya fedha inafaa, lakini sio Sunnah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pete?

Jibu: Hapana neno ikiwa ni pete ya fedha. Sio Sunnah. Lakini ni jambo linalofaa.

Swali: Imepokelewa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivaa pete ya dhahabu?

Jibu: Ndio, kisha akaitupa. Baada ya hapo akavaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pete ya fedha.

Swali: Dhahabu nyeupe?

Jibu: Hapana, fedha. Alipomuona bwana mmoja mkononi mwake yuko na pete ya dhahabu akaitupa na kusema:

“Anakusudiaje mmoja wenu kuweka kaa la moto mkononi mwake?”

Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pete ya dhahabu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23314/ما-حكم-لبس-الخاتم-للرجال
  • Imechapishwa: 23/12/2023