Kuuliza kuhusu vitu vilivyopotea msikitini

Swali: Ikiwa mtu atapoteza saa au kalamu msikitini anaweza kuuliza ndani ya msikiti?

Jibu: Udhahiri ni kuenea, kwa sababu makatazo ya kutangaza vilivyopotea yanahusu vilivyopotea na vyenginevyo; wanyama wanyama na vitu vingine pia. Hukumu ni moja. Kwa mfano kuuliza “Nani ameona nguo yangu? Nani ameona kitabu changu? Nani ameona viatu vyangu?” Hukumu ni moja kama ya vilivyopotea. Misikiti haikujengwa kwa dhumuni hili.

Swali: Ikiwa alipoteza ndani ya msikiti huohuo?

Jibu: Udhahiri ni kwamba asimame nje ya msikiti na kuuliza. Afanye hivo kwa kutendea kazi ueneaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24827/ماذا-يفعل-من-فقد-ضالة-في-المسجد
  • Imechapishwa: 20/12/2024