Kutumia mali ya mayatima kwa sababu ya kumuhijia baba yao

Swali: Mimi ni mlezi wa mayatima. Wako na mali yao ambayo nimewawekea. Je, ni halali kwangu kuwafanyia hajj kwa ajili ya baba yao kutoka katika mali yao? Wao ndio wanapenda nifanya hivo.

Jibu: Si halali kwa kwake kufanya hivo. Si halali kuhiji kwa mali ya mayatima kwa ajili ya baba yao. Kila kitu cha kujitolea basi si halali kutumia mali ya mayatima. Isipokuwa kitu kimoja tu; nacho ni Udhhiyah. Ikiwa kuacha kuchinja Udhhiyah ni jambo linanyongeza nyoyo zao, basi ni sawa akawanunulia mnyama  na akawachinjia. Ikiwa baba yao hakuhiji ile hajj ya kwanza ambayo ni faradhi, basi si wao wala mwingine yeyote hana haki ya mirathi mpaka kwanza atekeleze faradhi. Kwa sababu faradhi ni deni na deni linatekelezwa kwanza kabla ya mirathi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1214
  • Imechapishwa: 24/08/2019