Kumchelewesha maiti siku moja au mbili

Swali: Ni ipi hukumu ya kumchelewesha maiti siku moja au mbili kwa lengo ndugu zake waweze kuwahi kumswalia ambao ni watu wengi?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Harakisheni jeneza.”

Anatakiwa kuharakishwa kwenda kwenye kaburi lake na wala asibakizwe. [… sauti haisikiki vizuri… ] Maiti anatakiwa kuharakishwa na wale waliobaki watamuombea du´aa popote walipo na watamuombea msamaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (15) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-24-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 24/08/2019