Swali: Aliyeritadi katika Uislamu ananufaika kwa “laa ilaaha illa Allaah” akiisema wakati wa kufa?

Jibu: Akisema hali ya kuwa ni mwenye kutubia na ni mwenye Ikhlaasw kwa Allaah (´Azza wa Jalla) anakubaliwa tawbah yake ikiwa ni kabla ya kukata roho. Ama ikiisema ule wakati wa kukata roho haikubaliwi kutoka kwake, kazi imekwisha na ´ibaadah inakuwa haimuwajibikii tena kwake. Wakati huo hakukubaliwi lolote kutoka kwake. Lakini akiisema kabla ya kukata roho ilihali ni mwenye kuiamini na nia yake ni kutubu kwa Allaah, itakubaliwa kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014