Kutokwa na damu puani ndani ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu damu ikitoka puani mwa mtu wakati anaswali?

Jibu: Ikiwa ni ndogo basi ni yenye kusamehewa. Aiondoshe kwa kitambaa au kitu kingine. Na ikiwa ni nyingi basi akate swalah na ajisafishe nayo na itasuniwa kwake kurudi kutawadha kwa ajili ya kutoka nje ya tofauti za wanazuoni. Kisha baada ya hapo ataianza swalah mwanzo wake. Ni kama ambavo akipatwa na hadathi ambayo kuna maafikiano juu yake kama mfano wa kutokwa na upepo au mkojo, basi atatakiwa kuikata swalah kisha arudi kutawadha na kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/403)
  • Imechapishwa: 25/09/2021