Kuchelewesha swalah mwanzoni mwa wakati kwa sababu ya kazi

Swali: Sisi ni wafanyakazi katika shamba tunaswali sote pamoja faradhi kwa sababu msikiti uko mbali nasi kwa karibu 2 km na aidha hatusikii adhaana. Tunaadhini na kukimu shambani. Wakati mwingine pengine tukachelewesha swalah kutoka nje ya wakati wake kwa karibu nusu saa kwa sababu ya kazi. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno kuswali shambani ikiwa msikiti uko mbali nanyi. Vilevile hapana neno kuchelewesha swalah nusu saa au mfano wake kutoka katika ule wakati wake wa mwanzo. Lakini kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora zaidi. Isipokuwa joto likiwa kali katika swalah ya Dhuhr. Katika hali hiyo kuchelewesha ndio bora. Vivyo hivyo kundi wakikubaliana kuchelewesha ´ibaadah mwanzoni mwa ule wakati wake basi imamu naye anatakiwa kuafikiana naye. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akichunga mkusanyiko wa watu katika swalah ya ´ishaa; akiwaona wamekusanyika basi anaharakisha, na akiwaona wamechelewa naye anachelewesha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/380)
  • Imechapishwa: 25/09/2021