Ni lazima kwa bubu na kiziwi kufanya ´ibaadah?

Swali: Mtoto ambaye ni kiziwi na bubu anazingatiwa ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia kama mfano wa swalah au ni mwenye kupewa udhuru?

Jibu: Mtoto ambaye ni kiziwi na bubu akiwa amekwishafikia baleghe anazingatiwa ´ibaadah mbalimbali ni zenye kumuwajibikia kukiwemo swalah na nyenginezo na afunzwe yale yanayomlazimu kwa njia ya uandishi na kuashiria. Hayo ni kutokana na ueneaji wa dalili za Shari´ah zinazojulisha kwamba ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia ambaye amekwishabaleghe na akiwa na akili.

Kubaleghe kunapatikana kwa kufikisha miaka kumi na tano, kutokwa na manii kwa matamanio kwa kuota au kwa njia nyingine na kumea nywele za sehemu ya siri. Mwanamke anazidisha jambo la nne ambalo ni hedhi.

Ni lazima kwa mlezi wake kumtolea yale yanayomlazimu kama mfano wa zakaah na mengineyo ambayo ni haki ya mali. Ni lazima vilevile kwake amfunze yale asiyoyajua kwa zile njia zinazowezekana ili afahamu yale aliyomuwajibishia Allaah na kumuharamishia. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninapokuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”

Ambaye ´ibaadah zinamuwajibikia asiyesikia, asiyezungumza au ambaye amefikwa na uziwi na ububu vyote viwili ni lazima kwake kumcha Allaah vile awezavyo kwa kufanya yale mambo ya wajibu na kuacha mambo ya haramu. Ni lazima kwake kujifunza dini kwa kiasi cha uwezo wake kwa kuona, kuandika na kuashiria mpaka aelewe malengo.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/369)
  • Imechapishwa: 25/09/2021