Swali: Je, kumethibiti dalili kwamba kutokwa na damu kunachengua wudhuu´?

Jibu: Sijui kitu cha wazi kabisa. Isipokuwa ikiwa damu hiyo inatoka kwenye tupu, kama vile damu ya ugonjwa inayotoka kwenye uke wa mwanamke. Lakini ikiwa ni damu inayotoka kusikokuwa kwenye tupu, basi salama zaidi mtu atawadhe ikiwa ni nyingi. Damu ndogo ni yenye kusamehewa. Hata hivyo ikiwa ni nyingi salama zaidi atawadhe kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano ya wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23173/هل-خروج-الدم-ينقض-الوضوء
  • Imechapishwa: 18/11/2023