Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu kuwatukana Maswahabah

Swali: Kuwatukana Maswahabah ni ukafiri moja kwa moja au kuna upambanuzi?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba ni ukafiri. Kuwatukana kwa jumla au kuwachukia ni ukafiri. Hakuna anayewachukia isipokuwa kafiri. Wao ndio wabebaji wa Shari´ah.

Swali: Je, kuna tofauti kati ya Maswahabah wakubwa na wadogo?

Jibu: Kinachozingatiwa ni Maswahabah wote au wengi wao. Lakini kuwatukana baadhi yao mmojammoja – kama mfano wa Mu´aawiyah au mwengine – ni ufuska. Akimtukana mmoja katika wao anatakiwa kuaziriwa na kutiwa adabu.

Swali: Vipi akimtukana mmoja katika wale kumi walioahidiwa Pepo?

Jibu: Akimtukana ni ufuska. Anastahiki kutiwa adabu.

Swali: Lakini hawa wameshuhudiwa Pepo?

Jibu: Pengine kuna sababu zilizompelekea kutukana. Lakini hakuwatukana wote au wengi wao isipokuwa ni kwa sababu yuko na shaka katika dini yake na anaichukia dini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23172/حكم-من-سب-الصحابة
  • Imechapishwa: 18/11/2023