Kutoka nchi ya kikafiri na kuhajiri nchi ya kikafiri nyingine

Swali: Je, inajuzu kuhama kutoka katika nchi ya kikafiri na kwenda katika nchi ya kikafiri nyingine ilio na usahali kuliko hiyo ya kwanza na siwezi kufanya Hijrah kwenda katika nchi ya Kiislamu?

Jibu: Ndio, hili ni kwa njia ya kufanya uovu mdogo ili kuepuka uovu mkubwa. Maswahabah walihama kutoka Makkah kwa washirikina na wakahajiri kwenda kwa an-Najaashiy ambaye alikuwa ni mnaswara. an-Najaashiy alikuwa ni afueni na hamdhulumu yeyote kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (57) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-07.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020