Mara nyingi Fajr inampita kwa usingizi

Swali: Mtu huyu mara nyingi anapitwa na swalah ya Fajr na anaiswali baada ya kutoka wakati wake kwa sababu ya usingizi. Je, anapata dhambi kwa hilo na inahesabika ni katika unafiki?

Jibu: Haijuzu ikiwa atazoe kufanya hivi. Ama ikimpitikia baadhi ya nyakati, anataka kuamka na ameazimia kufanya hivo, lakini hata hivyo baadhi ya usiku usingizi ukamuia mzito pasi na kukusudia, huyu anapewa udhuru. Ama yule mwenye kuendelea kufanya hivi, haijuzu.

Isitoshe hulala wapi? Je, halali kati ya watu wengine, hana saa na alamu?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (57) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-07.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020