Swali: Ni ipi hukumu ya kutoka msikitini baada ya adhaana?
Jibu: Wakati Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuona bwana mmoja anatoka msikitini baada ya adhaana, akasema:
“Kuhusu huyu amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
Msingi ni kwamba maasi ni haramu. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا
“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[2]
Kwa ajili hiyo wanazuoni wamesema kuwa haijuzu kwa mtu kutoka msikitini baada ya adhaana isipokuwa kama kuna udhuru. Kwa mfano akatoka kutawadha kisha atarejea. Ikiwa anachelea kukosa swalah ya mkusanyiko, basi hapo hatakiwi muda wa kuwa hakushindwa na haja kubwa au ndogo. Ikiwa ameshikwa na haja kubwa au ndogo, basi atoke nje ya msikiti hata kama atakosa swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah wakati chakula kimeshaletwa au wakati mtu anazuia haja.”[3]
Tukikadiria kuwa mtu yuko msikitini na akashikwa na haja kubwa, haja ndogo au kutokwa na upepo, basi hapana vibaya kutoka kisha kurudia baadaye. Akiwahi swalah ya mkusanyiko ni vyema. Vinginevyo hapana vibaya kwake.
[1] Muslim.
[2] 33:36
[3] Muslim (560).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/200)
- Imechapishwa: 04/05/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/200)
Imechapishwa: 04/05/2026
https://firqatunnajia.com/kutoka-msikitini-baada-ya-adhaana/