Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Ama faradhi zake ni sita:
1 – Kuosha uso kukiwemo vilevile kusukutua na kupalizia. Mpaka wa uso ni pale nywele za kichwa zinapoanzia mpaka kwenye kidevu, na kuanzia kwenye sikio la kulia mpaka la kushoto.
2 – Kuosha mikono miwili mpaka kwenye visugudi.
3 – Kupangusa kichwa chote kukiwemo masikio.
4 – Kuosha miguu miwili mpaka kwenye vifundo vya miguu.
5 – Kuyafanya kwa kupangilia.
6 – Muwaalaah [kiungo kimoja kisiwahi kukauka kabla ya kuoshwa cha kufuatia].
Dalili ya hilo ni Kauli Yake (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَينِ
“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni.”[1]
Dalili ya kupangilia ni Hadiyth:
“Anza kwa alichoanza nacho Allaah.”[2]
Na dalili ya Muwaalaah ni Hadiyth ya mtu aliyeacha sehemu bila ya kuosha. Imepokelewa kwamba wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona mtu aliyeacha sehemu katika mguu wake kiasi cha dirhamu hakikufikiwa na maji, hivyo akamuamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kurudia na kutia [wudhuu´] upya[3].
Ni wajibu kusema “Bismillaah” mtu akikumbuka hilo.
MAELEZO
Sifa ya wudhuu´ imebainishwa ndani ya Kitabu cha Allaah na ndani ya Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) imekuja ndani ya Suurah ”al-Maa-idah” katika maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni.”
Maana ya maneno Yake:
ni kwamba mnapotaka kuswali huku mkiwa hamna twahara. Ni kama mfano wa maneno Yake:
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
“Unapotaka kusoma Qur-aan basi, omba ulinzi kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”[4]
Kwa maana ya kwamba unapotaka kusoma.
Kuhusu Sunnah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imekuja katika maneno na vitendo vyake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja na:
”Humraan (Radhiya Allaahu ´anh), mtumwa aliyeachiwa huru na ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye ameeleza ya kwamba alimuona ‘Uthmaan akiomba maji ya wudhuu´, ambapo akamimina juu ya mikono yake kutoka kwenye chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wa kulia kwenye maji, kisha akasukutua mdomo, akavuta maji puani na kuyapuliza, kisha akaosha uso wake mara tatu, mikono yake hadi kwenye vifundo mara tatu, kisha akapaka kichwa chake, kisha akaosha kila mguu wake mara tatu. Kisha akasema: “Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha kama wudhuu´ wangu huu na akasema: ”Yeyote atakayetawadha kama wudhuu´ wangu huu kisha akaswali Rak´ah mbili bila kujishughulisha na lolote, basi Allaah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia.’”
Ameipokea al-Bukhaariy (164) na Muslim (226).
Kuosha viungo mara tatu ndio wudhuu´ kamili. Hairuhusiwi kuzidisha zaidi ya mara tatu. Imepokelewa pia kutia wudhuu´ viungo mara mbilimbili na mara mojamoja. Hata hivyo wudhuu´ wa wajibu ni kuosha kila kiungo mara moja, kwa kuhakikisha maji yameenea.
[1] 05:06
[2] an-Nasaa’iy (2962). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Tamaam-ul-Minnah”, uk. 88.
[3] Abu Daawuud (175) na Ahmad (15595). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (168).
[4] 16:98
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 13-14
- Imechapishwa: 04/05/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 13-14
Imechapishwa: 04/05/2026
https://firqatunnajia.com/12-faradhi-sita-za-wudhuu/