Kutofunga kwa ambaye amesafiri kwenda ´Umrah katika Ramadhaan

Swali: Je, inafaa kwa muislamu kwenda ´Umrah katika Ramadhaan na akala katika safari yake au bora afunge na acheleweshe ´Umrah baada ya kumaliza kufunga?

Jibu: Bora ni yeye kufanya ´Umrah katika Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“´Umrah katika Ramadhaan inalingana na hajj.”

Kufanya ´Umrah katika Ramadhaan kuna shani ya kipekee:

“´Umrah katika Ramadhaan inalingana na hajj.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“´Umrah katika Ramadhaan ni kama kuhiji na mimi.”

Bi maana pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jambo lenye fadhilah kubwa.

Akisafiri amepewa khiyari; akitaka atakula anapokuwa njiani na akitaka atafunga. Jambo ni lenye wasaa. Vivyo hivyo pale atakapokuwa Makkah. Ikiwa atakaa Makkah siku chache kama vile siku mbili, siku tatu au siku nne basi inafaa kwake kutofunga kama ambavo inafaa vilevile kufunga. Lakini akiwa atakaa zaidi ya siku nne, basi atatakiwa kufunga Makkah na wala asile muda wa kuwa amekusudia kukaa Makkah zaidi ya siku nne. Ama ikiwa amekusudia kufanya ´Umrah kisha arudi, au atabaki siku moja, siku mbili au siku tatu, basi huyu anaruhusiwa kutofunga kama ambavo inafaa pia kufunga. Kwa maana nyingine amepewa khiyari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1815/حكم-الافطار-لمن-سافر-في-رمضان-للعمرة
  • Imechapishwa: 25/03/2023