Swali: Baadhi ya watu wa Peponi watamuona Allaah zaidi kuliko wengine?

Jibu: Wakazi wote wa Peponi watamuona. Hata hivyo wanatofautiana; baadhi yao wako juu zaidi na hivyo watamuona zaidi.

Swali: Mara ngapi?

Jibu: Nimesema baadhi yao watamuona zaidi kutegemea na kumcha kwao Allaah, kumwamini kwao na ngazi zao Peponi. Miongoni mwao wako ambao watamuona kwa makisio ya asubuhi na jioni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22748/هل-يتفاوت-المومنون-في-روية-ربهم-بالجنة
  • Imechapishwa: 17/08/2023