Swali: Ni ipi hokumu ya kutoa mchele katika Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Hapana shaka juu ya kufaa kwake. Hii leo pengine mchele ndio kitu bora anachoweza kutoa mtu katika Zakaat-ul-Fitwr. Kwa sababu ndio chakula kinacholiwa zaidi leo. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Fitwr tulikuwa tukitoa Swaa´ ya chakula. Chakula chetu kipindi hicho kilikuwa shayiri, zabibu na maziwa makavu.”

Si kwamba kinachotolewa ni hiki kilichotajwa hapa juu peke yake. Lakini ni kwa sababu ndio ambacho kilikuwa chakula chao kipindi hicho.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/283)
  • Imechapishwa: 06/05/2021