Miongoni mwa mambo ambayo ni muhimu, na khaswa inapokuja kwa wasichana, ni kwamba mtu anatakiwa kuchunga ni namna gani msichana wake anaenda masomoni. Utawaona baadhi ya wasichana wanaomba mavazi bora na mazuri kabisa. Na kila kunapotoka mtindo fulani basi anamuomba mama yake amnunulie ili apate kujifakharisha mbele ya marafiki zake wa klasini. Hili ni kosa; ni kosa ambalo ni kubwa.

Nilikuwa nafikiria kuwa mamlaka ndio inayoamrisha kwamba kila mmoja avae mavazi kama hayo. Ikiwa nidhamu ndivo inavosema, basi ni lazima kuifuata. Haijuzu kwa mtu akaitumia vibaya. Kwa sababu watawala wakiamrisha jambo ambalo ndani yake hakuna kumuasi Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi lililo la lazima kwa ummah waifuate. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]

Jambo jengine muhimu la kuangalia ni mtu atazame ni mtu gani anayekwenda na msichana wake au dada yake kwenda naye masomoni. Akiwa ataenda pamoja na dereva basi ni lazima aweko ndani ya gari ima mwanamke mwingine au Mahram. Haijuzu kwa dereva wa kiume kukaa faragha na mwanamke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamme hawi faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao huwa ni shaytwaan.”[2]

Unafikiria kutokea kitu gani ikiwa watu wawili ambapo watatu wao ni shaytwaan?

[1] 04:59

[2] at-Tirmidhiy (1171).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (60 A)
  • Imechapishwa: 04/12/2020