Swali: Ni ipi hukumu ya kuchonga nyusi na kuondosha nywele za usoni[1] kwa wanawake?

Jibu: Kuchonga nyusi wala kujisafisha ngozi ya mwili haijuzu. Huku ni kubadilisha maumbile ya Allaah (´Azza wa Jall). Mwenye kuchonga nyusi amelaaniwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa. Ni mwanamke mwenye kuondosha nyusi zake au baadhi yake. Hali kadhalika inahusiana na kusafisha ngozi ya mwili. Ni sawa akajipodoa kwa vipodozi vinavyoruhusiwa tofauti na kujisafisha ngozi ya mwili jambo ambalo ni njia moja wapo ya kubadilisha maumbile ya Allaah.

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Chemical_peel

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020