Kutawadha zaidi ya mara tatu bila kukusudia

Swali: Imekuja katika Hadiyth:

“Hakika yule ambaye atazidisha katika wudhuu´ juu ya kunawa mara tatu basi kwa hakika amechupa mpaka, amedhulumu na amefanya vibaya.”

Je, anapata dhambi ambaye baadhi ya nyakati atazidisha pasi na kukusudia isipokuwa amefanya hivo kwa kuchelea pengine ameacha sehemu kidogo na anaingia katika matishio haya?

Jibu: Hapana, akiona sehemu kidogo basi ni lazima aioshe. Mambo ni sahali. Ni lazima akamilishe. Hajakamilisha kunawa mara tatu. Ikiwa kuzidisha kunatokana na wasiwasi au dhana peke yake basi haitofaa kuzidisha zaidi ya mara tatu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 04/12/2020