Swali: Je, inafaa kutamka nia wakati wa kuchinja Udhhiyah?

Jibu: Kilichosuniwa ni yeye kutamka na kusema:

اللهم إنها منك ولك هذه كذا ضحية عن فلان

“Ee Allaah! Hakika kinatokana Nawe na kwa ajili Yako. Ni kichinjwa cha fulani.”

Hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi  wa sallam) alivokuwa akifanya. Kadhalika kuhusiana na kichinjwa cha Hadiy. Aseme:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Ni sawa pia akitaja jina la mchinjiwa. Vinginevyo inatosha kuweka nia. Aseme:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Ni sawa pia ikiwa atasoma:

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

“Sema: “Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”[1]

Ni sawa pia akisema:

اللهم تقبل من فلان

“Ee Allaah! Mkubalie fulani.”

Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo ni lazima alete Tasmiyah:

باسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

Bora aseme yote kwa pamoja:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Kuhusu kichinjwa cha Udhhiyah aseme:

“Ni cha fulani.”

Hivo ndivo alivofanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Udhhiyah:

عن محمد وآل محمد

“Ni kwa ajili ya Muhammad na familia ya Muhammad.”

Kuhusu kichinjwa cha Hadiy inatosha kuweka nia kama ni Hadiy ya hijjah ya Tamaattu´ au Qiraan au kama ameacha jambo la wajibu au amefanya jambo alilokatazwa. Inatosha kuweka nia na kusema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

[1] 06:162

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18210/حكم-التلفظ-بالنية-عند-ذبح-الاضحية-والهدي
  • Imechapishwa: 10/06/2024