133 – ´Umar al-Faarisiy ametukhabarisha: Ibn-ul-Latiy ametuhadithia: Abul-Waqt ametuhadithia: ad-Daawuudiy ametuhadithia: Ibn Hammuuyah ametuhadithia: ´Iysaa bin ´Umar ametuhadithia: ad-Daarimiy ametuhadithia: Muhammad bin al-Fadhwl ametuhadithia: as-Swa´iq bin Hazn ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin al-Hakam, kutoka kwa ´Uthmaan bin ´Umayr, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa Ibn Mas´uud ambaye amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu Nafasi ya kusifiwa. Akajibu: ”Hiyo ni ile siku ambayo Allaah (Ta´ala) atashuka juu ya Kursiy Yake ambayo itanguruma kama inavyonguruma tandiko jipya kutokana na kishindo Chake. Ni kama masafa yaliyopo kati ya mbingu na ardhi. Mtaletwa hali ya kuwa peku, uchi na pasi na kutahiriwa. Mtu wa kwanza kuvishwa nguo atakuwa Ibraahiym (´alayhis-Salaam). Allaah atasema: ”Mvisheni nguo kipenzi changu mwandani.” Apewe vitambaa viwili vyeupe kutoka Peponi. Kisha avishwe. Halafu nitasimama upande wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall), maeneo ambayo watanionea wivu wa mwanzo na wa mwisho.”[1]

Wanazuoni wamemdhoofisha ´Uthmaan Abul-Yaqdhwaan. Kikosi wameipokea kutoka kwa as-Saa-iq.

134 – Zam´ah bin Swaalih amepokea kutoka kwa Salamah bin Wahraam, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”

”Allaah atakuja siku ya Qiyaamah katika vivuli vya mawingu vilivyotawanyika.”

Wengi wameipokea kutoka kwa Zam´ah. Wengine wameipokea vilevile kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo si sahihi.

135 – Huudhah ameeleza: ´Awf ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Minhaal, kutoka kwa Shihr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Wakazi wa mbingu ya saba ni wengi maradufu kuliko wakazi wa mbingu ya sita na wakazi wa ardhini. Allaah awajilie wakati ambapo wamekaa kwa magoti yao wamejipanga safu.”

136 – Ibn-ul-Mubaarak amesema: Raashid al-´Attwaar ametuhadithia: Shihr bin Hawshab amenihadithia: Nimemsikia Ibn ´Abbaas akisema:

”Allaah atakuja siku ya Qiyaamah katika vivuli vya mawingu.”

137 – Ishaaq bin Sulaymaan ar-Raaziy amepokea kutoka kwa Jabr, kutoka kwa Shihr bin Hawshab, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Allaah atawateremkia Malaika. Ataiweka ´Arshi na mizani mkononi Mwake. Aseme: ”Enyi Malaika! Enezeni kati ya viumbe! Naapa kwa utukufu Wangu! Haitokuwa karibu Yangu dhuluma ya mwenye kudhulumu.”

”Kusanyeni kati ya viumbe!”

138 – Muhammad bin ´Adiy: ´Awf ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Minhaal: Shihr amenihadithia: Ibn ´Abbaas ametuhadithia:

”Itapokuwa siku ya Qiyaamah ardhi itasawazishwa kama ngozi na watu watakusanywa katika uwanja mmoja… na Allaah (Ta´ala) atakuja wakati ambapo ummah utakuwa umekaa kwa magoti.”

Kikosi wameipokea kutoka kwa ´Awf.

139 – Sa´iyd bin Bashiyr amesema: al-Qaasim bin al-Waliyd ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Allaah atashuka siku ya Qiyaamah katika vivuli vya mawingu.”

[1] ad-Daarimiy (2/325), Ahmad (1/398-399), at-Twabariy (15/98-99), al-Haakim (4/575) ambaye ameisahihisha na at-Twabaraaniy (10/98-99).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 140-145
  • Imechapishwa: 10/06/2024