131 – Ismaa´iyl bin ´Ubayd bin Abiy Kariymah amesema: Muhammad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Abdir-Rahmaan Khaalid bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa Zayd bin Abiy Aniysah, kutoka kwa al-Minhaal bin ´Amr, kutoka kwa Abu ´Ubaydah bin ´Abdillaah bin Mas´uud, kutoka kwa Masruuq: ´Abdullaah ametuhadithia, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

”Allaah atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho katika siku ya wakati maalum. Watasimama miaka arobaini na macho yao yakiwa yametazama juu wakisubiri kuhukumiwe. Allaah atashuka katika vivuli vya mawingu, kutoka katika ´Arshi kwenda katika Kursiy. Ndipo ataita mwitaji: ”Enyi watu! Je, hamko radhi kwa Mola wenu amwache kila mmoja katika nyinyi ajichukulie kile alichokuwa akikichukua na kukiabudu duniani? Je, hivo ni kufanya uadilifu kwa Mola wenu?” Watasema: ”Ndio.” Wataondoka na watafanyiwa mfano wa vile walivyokuwa wakiviabudu. Baadhi yao wataliendea jua, wengine watauendea mwezi. Wale waliokuwa wakimwabudu ´Iysaa watafanyiwa mithili ya shaytwaan ´Iysaa, na wale waliokuwa wakimwabudu ´Uzayr, watafanyiwa mithili ya shaytwaan ´Uzayr. Abaki Muhammad na ummah wake. Ndipo Mola ajimithilishe, awajie na awaambie: ”Ni kwa nini hamuondoki kama walivyoondoka wengine?” Watasema: ”Sisi tunaye Mola ambaye bado hatujamuona.” Ndipo aseme: ”Je, mtamjua mkimuona?” Watasema: ”Ndio. Kuna alama baina yetu sisi na Yeye; tutapoiona tutamjua.” Atasema: ”Ni ipi?” Watasema: ”Atafunua muundi Wake.” Hapo ndipo Allaah atafunua muundi Wake. Wale wote ambao mgongoni mwao kuna uti wa mgongo wataporomoka kumsujudia, na wale wote ambao migongo yao ni kama pembe za ng´ombe watataka kuporomoka kusujudu, lakini hawatoweza:

وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ

”… na hali walikuwa wakiitwa kusujudu walipokuwa wazima wa afya.”[1]

Ameipokea Ibn Waarah, ´Abdullaah bin Ahmad na wengineo kupitia kwa Ismaa´iyl ambaye alikuwa anaaminika.

ath-Thawriy na wengineo pia wameipokea kupitia kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa Abuz-Za´raa’, kutoka kwa ´Abdullaah kwa tamko lisemalo:

”Allaah atajimithilisha mbele ya viumbe kisha baadaye awajie katika sura Yake.”

Wamepokea kutoka kwa al-Minhaal pia ´Abdul-A´laa bin Abiyl-Musaawir na Yaziyd bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daalaaniy.

132 – Wameipokea zaidi ya mmoja kutoka kwa Zayd bin Abiy Aniysah yakiwa kama maneno ya Swahabah. al-A´mash amepokea kutoka kwa al-Minhaal bin ´Amr, kutoka kwa Abu ´Ubaydah Qays bin as-Sakan, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

”Pindi watu watapokusanywa, watasimama miaka arobaini na macho yao yakiwa yametazama juu… ”[2]

[1] 68:43

[2] Jaamiy´-ul-Bayaan (25/29).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 135-139
  • Imechapishwa: 10/06/2024