28. Hadiyth ”Ndipo Allaah awajie katika sura… ”

Hadiyth ya kumi na mbili

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“… na takapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”[1]

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ

“Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawajie au awafikie Mola?”[2]

127 – Yuusuf bin Abiy Naswr ametukhabarisha: al-Husayn bin Abiy Bakr ametuhadithia: Abul-Waqt as-Sijziy ametuhadithia: Abul-Hasan ad-Daawuudiy ametuhadithia: Abu Muhammad bin A´yun ametuhadithia: Abu ´Abdillaah al-Farabriy ametuhadithia: Abu ´Abdillaah al-Bukhaariy ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia: al-Layth ametuhadithia, kutoka kwa Khaalid bin Yaziyd, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Hilaal, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa Abu Sa´iyd ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Uombezi:

”Ndipo Allaah awajie katika sura isiyokuwa sura aliyowajilia mara ya kwanza. Waseme: ”Mimi ni Mola wenu.” Watasema: ”Wewe ni Mola wetu.” Hakuna watakaomzungumzisha isipokuwa tu Manabii.”[3]

128 – Hammaad bin Salamah amesimulia kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa Yuusuf bin Mihraan, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

”Mola (Tabaarak wa Ta´ala) atawajia wale Malaika walio karibu. Watakuwa wengi kuliko wakazi wa mbingu na ardhini.”

Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

129 – Imethibiti kuwa Mujaahid amesema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ

“Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”[4]

”Haya sio mawingu. Hakuna waliopata jambo hilo isipokuwa tu wana wa israaiyl wakati wa safari yao ya jangwani. Ndicho atachokuja nacho Allaah siku ya Qiyaamah.”

130 – Imesihi kutoka kwa Abu Sa´iyd na wengineo ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ndipo awajilie Allaah katika sura nyingine isiyokuwa ile wanayoijua.”[5]

[1] 89:22

[2] 6:158

[3] al-Bukhaariy (806), Ibn ´Awaanah, Muslim, Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd” (1/376) na al-Haakim.

[4] 2:210

[5] al-Haakim (4/570).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 133-135
  • Imechapishwa: 10/06/2024