Kutabaruku kwa Maswahabah kwa athari za Mtume

Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anh) walikuwa wakitabaruku kwa mate na majasho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ilikuwa ni mazowea yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi anapoamka alfajiri anakuja na chombe kilicho na maji ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ananawa mikono yake ndani ya maji yale na anampa mtoto maji yake na anaenda nayo kwa familia yake ili watabaruku kwa athari ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anatawadha Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakipigania maji yale, fadhilah za yale maji, ili watabaruku kwayo. Hali kadhalika wanafanya kwa majasho na nywele zake.

Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa), ambaye ni mmoja katika wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alikuwa na chombo cha fedha ambapo ndani yake mlikuwa nywele zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakijitibu kwazo. Wanachukua nywele mbili au tatu na kuziweka kwenye maji kisha yale maji wanayatikisa ili waweze kutabaruku kwayo. Hili ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/269-270)
  • Imechapishwa: 15/03/2023