Baadhi ya watu wanakuwa na khiyari ya kuteua mfanya kazi ambaye ni muislamu na kafiri, lakini hata hivyo anamchagua kafiri. Nyoyo zimepinda na kupotea. Shaytwaan anawapambia matendo yao. Wanasema kwa uongo na uzushi ya kwamba kafiri ni mwenye kufanya kazi kwa uaminifu na ukweli kuliko muislamu. Ninaomba kinga kwa Allaah. Wanasema kuwa kafiri hatoswali wakati wa kazi bali ataendelea kufanya kazi wakati wa swalah. Hahitajii kwenda katika ´umrah wala hajj na hafungi. Siku zote atakuwa kazini. Jambo hili [la kuwachukia makafiri kwa ajili ya Allaah] halimwambii kitu pamoja na kwamba Mola wa ardhi na mbingu anasema:

وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ

“Na wala msiwaozeshe [wanawake wa Kiislamu] wanaume washirikina mpaka waamini na mtumwa muumini ni bora kuliko mshirikina ijapo akikupendezeni – hao wanaitia katika Moto na Allaah anaitia katika Pepo na msamaha kwa idhini Yake.”[1]

Ni wajibu kwenu ndugu kuwanasihi ndugu zenu ambao wamedanganyika na shaytwaan amewapambia kitendo cha kuwaleta wafanya kazi makafiri katika nchi yetu. Ni wajibu watambue ya kwamba kwa kufanya hivo ni kuwapa nguvu makafiri dhidi ya waislamu.

[1] 02:221

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/266-267)
  • Imechapishwa: 15/03/2023