Swali: Mtu hatokutana na wakati uliokatazwa akiswali mpaka atakapoingia Khatwiyb siku ya ijumaa?

Jibu: Siku ya ijumaa hakuna wakati uliokatazwa. Hakuna wakati uliokatazwa katika kipindi cha mchana. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekokoteza kuswali mpaka atakapoingia imamu. Kungelikuwa na wakati uliokatazwa basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelibagua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22603/حكم-النافلة-يوم-الجمعة-حتى-دخول-الخطيب
  • Imechapishwa: 08/07/2023