Kuswali nyuma ya imamu unayeona wudhuu´ wake umechenguka

Swali: Ikiwa mswaliji anaona kuwa nyama ya ngamia inachengua wudhuu´ lakini imamu haoni kuwa inachengua.

Jibu: Unaswali nyuma yake. Hili ni eneo la Ijtihaad. Lakini ukidhihirikiwa kufanya jambo linalochengua wudhuu´ kupitia sauti au harufu, licha ya hivo akaendelea kuwaswalisha watu, hapana. Lakini jambo ambalo linatokana na Ijtihaad, kama kumgusa mwanamke na kula nyama ya ngamia yeye akaona kuwa hakuchengui wudhuu´, kuswaliwe nyuma yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25091/حكم-امامة-من-لا-يرى-نقض-الوضوء-باكل-لحم-الجزور
  • Imechapishwa: 01/02/2025