Asiyeweza kurudisha haki za wenyewe

Swali: Kuhusu sharti la mwisho la masharti ya tawbah ambalo ni kurejesha haki ya uliyemdhulumu. Mimi ni masikini ambaye siwezi kurejesha haki za vitu vya watu nilivyoiba.

Jibu: Atake idhini kutoka wao. Ikiwa anashindwa kufanya hivyo, basi Allaah anajua azma yake kikamilifu. Ikiwa ametia azma ya hilo, basi Allaah atamsamehe. Ikiwa ameshindwa na hawakukusamehe, basi Allaah atakusamehe. Ikiwa umetubu kwa uaminifu; kwa sababu ambaye ameshindwa kikweli ni kama aliyetekeleza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25089/حكم-من-لا-يستطيع-رد-المظالم
  • Imechapishwa: 01/02/2025