Kuswali nyuma ya imamu anayeapa kwa asiyekuwa Allaah

Swali: Je, inajuzu kuswali nyuma ya ambaye anaapa kwa asiyekuwa Allaah, anavaa hirizi na ana imani fulani kwa Shaykh miongoni mwa Mashaykh wa Suufiyyah?

Jibu: Kuapa kwa asiyekuwa Allaah inaweza kuwa shirki kubwa na inaweza vilevile kuwa shirki ndogo kutegemea na kile kilicho kwenye moyo wa muapaji. Kadhalika hirizi kuna ambayo ni shirki kubwa na nyingine shirki ndogo. Vilevile kuwa na imani kwa Shaykh wa Suufiyyah hukumu ni yenye kutofautiana kutegemea na imani yake. Wewe hukubainisha hali yake katika swali. Lakini hata hivyo inatakiwa kumnasihi imamu huyu kutokana na yale anayofanya ambayo hayamridhishi Allaah; akikubali nasaha vizuri, la sivyo aswali nyuma ya mwingine.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/233)
  • Imechapishwa: 24/08/2020