Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kutumia aina yoyote ile ya Ruqyah?

Jibu: Ruqyah inayojuzu ni ile isiyokuwa na shirki; kama Suurah na Aayah za Qur-aan na Adhkaar zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haijuzu kutumia yale yaliyo na shirki; kama kumkinga mgonjwa kwa majina ya majini na watu wema na kwa [maneno] yasiyofahamika maana yake kwa kuchelea isijekuwa shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ni sawa kutumia Ruqyah midhali hakuna shirki.”

Ameipokea Muslim.

Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kuomba kwa Majina ya Allaah (Ta´ala) ili kuponya maradhi?

Jibu: Inajuzu kufanya hivo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا

“Allaah ana majina mazuri mno, hivyo basi muombeni kwayo.” (07:180)

Vilevile kwa kuthibiti hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwasomea baadhi ya watu kwa kusema:

اللهم رب الناس، أذهب البأس، واشف، أنت الشافي لا شفاء إلا شفاؤك، شفاءً لا يغادر سقماً

“Ee Allaah! Mola wa watu ondosha haya maradhi na mponye wewe ni mponeshaji hakuna shifaa isipokuwa shifaa yako, ponyo ambalo halitoacha maradhi.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/167)
  • Imechapishwa: 24/08/2020