Inafaa kuapa kwa asiyekuwa Allaah?

Swali: Je, inajuzu kuapa kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Haijuzu kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tanabahini! Allaah anakukatazeni kuapa kwa baba zenu. Mwenye kutaka kuapa basi naape kwa Allaah au anyamaze.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Katika upokezi wa Abu Daawuud na an-Nasaa´iy kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) Marfuu´ah imekuja:

“Msiape kwa baba zenu wala mama zenu na wala msiape kwa Allaah isipokuwa muwe ni wakweli.”

Abu Daawuud na at-Tirmidhiy wamepokea kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru na kufanya shirki.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/231)
  • Imechapishwa: 24/08/2020