Kuswali ndani ya maktabah iliyo karibu na msikiti

Swali: Je, inajuzu kuswali kwenye maktabah mkusanyiko pamoja na kuzingatia ya kwamba msikiti uko karibu na maktabah?

Jibu: Haijuzu kwa ambaye msikiti uko pambizoni mwake kuswali ndani ya maktbah. Ni wajibu kwake kutoka  ili aswali pamoja na mkusanyiko. Ni kama ambavyo haijuzu pia kuswali nyumbani, bali ni wajibu kwake kutoka ili aswali pamoja na mkusanyiko.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1107/يصلي-في-المكتب-رغم-قربه-من-المسجد
  • Imechapishwa: 25/01/2026