Kuswali naafilah baada ya Dhuhaa mpaka wakati wa Dhuhr

Swali: Nikiswali Rakaa mbili za Dhuhaa baada ya jua kuchomoza, halafu nikaendelea kuswali Swalah zingine za Sunnah kabla ya jua kusimama inajuzu na inakuwa ni katika Swalah ya Dhuhaa?

Jibu: Ndio. Swali idadi utakayo. Swali idadi utakayo mpaka pale ambapo jua litasimama juu ya vichwa, hapo ndio usimame. Swali idadi utakayo. Ni sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14705
  • Imechapishwa: 19/04/2015