Kuswali na saa ilio na picha au msalaba

Swali: Baadhi ya saa kwa ndani ziko na picha za baadhi ya wanyama. Je, inafaa kuswali nazo? Vivyo hivyo inafaa kuswali na saa ilio na msalaba?

Jibu: Ikiwa picha kwenye saa iko kwa ndani na haionekani basi hapana vibaya. Lakini ikiwa inaonekana nje ya saa au inaonekana kwa ndani wakati anapoifungua, haitofaa. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha yoyote isipokuwa umeiharibu.”

Vivyo hivyo msalaba. Haijuzu kuvaa saa ambayo iko na msalaba isipokuwa baada ya kuisugua au kuifuta kwa rangi au kitu kingine mfano wake. Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ya kwamba alikuwa haoni kitu kilicho na msalaba isipokuwa hukifuta.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… isipokuwa hukikata.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/388)
  • Imechapishwa: 03/10/2021