Hukumu ya kufunika mabega ndani ya swalah

Swali: Baadhi ya watu wanaswali swalah ya faradhi na juu ya mabega yao hakuna kitu kinachowafunika na khaswa masiku ya hajj wakati wa Ihraam. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Akiwa hana uwezo basi hakuna dhambi juu yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Nguo ikiwa pana basi jifunike kwayo na ikiwa ni ndogo basi iweke kwa chini kama kikoi.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Lakini mtu akiwa na uwezo wa kufunika mabega yote mawili au limoja wapo, basi ni lazima kwake kuyafunika yote mawili au limoja wapo kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Akiacha kufanya hivo basi swalah yake haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiswali mmoja kwenye nguo moja ilihali hakuna juu ya mabega yake kitu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/415)
  • Imechapishwa: 03/10/2021