Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kutolingania katika Tawhiyd ili kuepuka matatizo

Swali: Kuna mtu analingania katika Uislamu katika maeneo ambayo Ahl-ul-Bid´ah wako wengi. Analingania katika matendo bora badala ya Tawhiyd ili kuepuka matatizo. Je, inafaa?

Jibu: Hili linatokana na kwamba malengo ya ulinganizi ni uongofu. Akiona kuwa anaweza kuwaongoza pasi na kuanza kuwakemea makosa yao ya Tawhiyd, sambamba na hilo amenuia kuzungumza Tawhiyd huko baadaye, lakini ametaka kwanza kuwatuliza kwa kuzungumzia swalah, zakaah, swawm na hajj kisha baada ya hapo aende hatua kwa hatua katika Tawhiyd, basi nataraji kwamba hakuna neno.

Hata hivyo ikiwa hataki kuzungumzia Tawhiyd kabisa kwa sababu inapelekea katika shari na kadhalika, haijuzu. Lakini akifanya hiyo ni njia inayopelekea kuzungumzia Tawhiyd ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (167 B)
  • Imechapishwa: 03/10/2021