Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa haijuzu kuswali na flana. Je, ni sahihi?

Jibu: Sio sahihi. Kwa sababu uchi wa mwanaume ni baina ya kitovu na magoti yake wakati anaposwali. Kifua, mgongo wake na mabega yake sio katika uchi. Imesihi ya kwamba Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliswali na shuka yake ya chini na akaining´iniza juu shuka yake ya juu. Bwana mmoja akamuuliza juu ya hilo ambapo akasema:

“Nimefanya hivo ili aone mpumbavu kama wewe.”[1]

Hilo linafahamisha kuwa inafaa. Hata hivyo bora ni yeye kufunika mabega yake. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiswali mmoja wenu ndani ya nguo moja pasi na kuwa na chochote juu ya bega lake.”[2]

Kufanya hivi ndio bora. Ama kusema kwamba swalah haisihi, sio sahihi. Aidha neno “chochote” linaashiria kwamba anaweza kuweka chochote, ijapo kidogo.

[1] Ahmad (3/335).

[2] al-Bukhaariy (359) na Muslim (516).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/266)
  • Imechapishwa: 14/06/2026