Ami anatoa zakaah ya watoto wa ndugu yake bila ya utambuzi wao

Swali: Baada ya bwana mmoja kufa na akaacha watoto wengi, kaka na ami yake wakachukua jukumu la kuwahudumia na kuwatolea zakaah zao. Hivi sasa watoto wamekuwa wakubwa; wasichana wameolewa na baadhi ya wanaume wanafanya kazi na wengine wanasoma. Je, inafaa kwa ami yao kuwatolea zakaah yao pasi na ya wao kujua, khaswa kwa kuzingatia kwamba yeye ndiye bado yuko na mirathi yao?

Jibu: Watoto wakishabaleghe na wakawa wakomavu na wenye akili ambao wanaweza kujiendeshea mali yao, unafutika usimamizi wa ami yao isipokuwa ikiwa wao wenyewe watamuwakilisha. Kwa maana hiyo haifai kwake kuwatolea zakaah yao isipokuwa kwa baada ya idhini yao.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/309)
  • Imechapishwa: 14/06/2026