Kuswali mbele ya mlalaji ambaye anajigeuzageuza

Swali: Je, kuna dalili inayokataza kuswali nyuma ya aliyelala?

Jibu: Hapana, hapana vibaya kufanya hivo.

Swali: Anajigeuzageuza ilihali amelala?

Jibu: Haidhuru.

Swali: Hakuzingatiwi kuwa ni kupita mbele ya mswaliji?

Jibu: Hapana, hakuzingatiwi kuwa ni kupita mbele ya mswaliji.

Swali: Kutoka kwake [´Aaishah] mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzingatiwi ni kupita?

Jibu: Kutoka kwake hakuzingatiwi ni kupita. Unaweza kutoka kwenye godoro, ukatoka kwa upande wa kichwa chake.

Swali: Anasema kuwa alitoka upande wa miguu yake?

Jibu: Ni mamoja upande wa miguu yake au kichwa chake. Yote ni mamoja. Hakuitwi kuwa ni kupita. Kupita ni kule ambako mtu anatoka upande huu anaenda upande ule.

Swali: Imetajwa katika baadhi ya Hadiyth kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa juu ya kitanda. Je, si kitanda chote…

Jibu: Yeye yuko juu ya kitanda. Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposujudu basi yeye [´Aaishah] anakunja miguu yake mpaka inagusana na miguu yake na yeye amelala.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23670/حكم-الصلاة-خلف-الناىم-وتقلبه-امام-المصلي
  • Imechapishwa: 26/03/2024