Ibn Baaz kuhusu kuashiria kidole baina ya sijda mbili

Swali: Maoni sahihi kuhusu kuashiria kidole kidogo katika kikao baina ya Sujuud mbili na kutikisa kidole kidogo?

Jibu: Ni Sunnah katika Tashahhud. Atapokuwa ameketi baina ya sijda mbili ataweka mikono yake juu ya mapaja yake au juu ya magoti yake. Upokezi huo unahitaji kuangaliwa vyema, kwa sababu unapingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh.

Swali: Mtu hawezi kusema kuwa baadhi ya nyakati ni Sunnah kuashiria kidole?

Jibu: Kinachotambulika katika Hadiyth Swahiyh ni kwamba kinatandazwa juu ya mapaja na magoti baina ya Sujuud mbili. Kidole cha shahaadah kitaashiriwa katika Tashahhud.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23669/ما-السنة-في-هيىة-الاصابع-بين-السجدتين
  • Imechapishwa: 26/03/2024